Je unajua Umuhimu wa Kutunza Kumbukumbu za Uzoefu wa Kazi yako?

0
221 views
  • Tunza nyaraka za uzoefu wako

  Kuna baadhi ya wafanyakazi wako tayari kuonyesha kumbukumbu za uongo ili waweze kubaki kwenye nyadhifa zao au kupata kazi wanazotaka.  Kwahiyo mwajiri anahitaji ushahidi wa uzoefu wako. Unapotunza nyaraka za uzoefu wako pamoja na taaluma uliyonayo huo ni ushahidi mzuri hasa unapokuwa kwenye nyaraka halisi kama barua za pongezi au kuwa mfanyakazi bora pamoja na yeti vya kutambua utendaji wako mzuri wa kazi.

   1. Weka nyaraka za maandishi kwa kazi zote ulizowahi kufanya
    Je nyaraka hizo ziwe zimeambatanishwa na nini? (1) Jina na anuani ya Mwajiri,
    (2) Majukumu uliyokuwa unafanya, (3) Kazi maalumu, (4) Sababu ya kuondoka, (5) Jina na anuani ya mtu ambaye anaweza kukudhamini au kuwa shuhuda wa nyaraka hizo
   2. Kila cheti unachopata kitunze 
    Hata taaluma ndogo ndogo kama, cheti cha kujifunza mafunzo ya huduma ya kwanza, semina na mafunzo ya ndani. Ni ushahidi na udhibitisho kwamba una uzoefu na una moyo wa kujifunza.
   3. Mwombeni mfanyakazi mwenzako au msimamizi wako wa karibu kukuandikia barua ya wazi
    Barua ya wazi ni ushahidi yenye kichwa cha habari “Kwa Yeyote anayehusika”. Hii yote ni kwasababu wafanyakazi wenzako huwa wanaondoka , wengine wanaondoka ghafla. Msimamizi wako wa karibu anaweza kuacha kazi na kuendelea sehemu nyingine na mara nyingine ikawa vigumu kumpata.
   4. Barua yoyote ya kukudhamini na kukudhibitisha zitunze.
    Kama hizo barua zilitumwa kuja kwenye kampuni hiyo unayofanyia kazi usiogope kuziomba hata wakupatie nakala kwa ajili ya kumbukumbu zako.
   5. Hakikisha unatunza mawasiliano ya msimamizi wako wa karibu kikazi pamoja na wafanyakazi ulio karibu nao kwa ajili ya baadaye.
    Kuna watu wengine watashukuru kwa huduma nzuri uliowafanyia kwa cutup kwa msimamizi wako wa karibu na hata pale utakapokuwa umeondoka, hivyo unapokuwa na mawasiliano mazuri wanaweza kukutumia barua au barua pepe hivyo kukuongezea nguvu kwenye ushahidi wa utendaji wako wa kazi.
   6. Hakikisha kila kitu kinachokuhusu unawake kumbukumbu zake. haijalishi hicho kitu ni kidogo kiasi gani, weka kumbukumbu kitakusaidia