Watu wabunifu na wenye uwezo wa kutekeleza ndio wenye mafanikio

0
211 views

Kuna watafiti wengi wa kisayansi ambao wamekuja na njia mbalimbali namna ambavyo unaweza kuboresha ubunifu wako. Njia hizo zinaweza kutumika mahali popote na kwa mtu yeyote mwenye uelewa na anayetaka kuboresha anachokifanya.

1. Usifikiri kwamba mafanikio yanakuja kwa Bahati

Kuna watu wengi wanaamini kwenye bahati na kuona kwamba kuna watu wenye bahati na watu wengine hawana bahati. Lakini zebu fikiri kwamba unaaamua kukaa tu na ukasubiri bahati ikujie? Unahitaji kufanya kitu au kufanya kazi fulani ndipo fulsa huanza kujitokeza za kukupeleka kiwango kingine. Mtaalamu mmoja alisema bahati huwapata waliojiandaa akili zao, kama umejiandaa kufanya kitu fulani labda ni biashara au kazi au michezo fulani hivyo fulsa zitakufuata kulingana na ulivyojiandaa. Watu wengi wakubwa au maarufu, wengi wao walipokuwa wadogo walikuwa na akili inayojitegemea na walikuwa na uwezo wa kuzifuata ndoto zao. unapopata ujasiri na kuamini unaweza kufanya kitu cha muhimu au kutatua tatizo muhimu utajikuta unaweza.

2. Huwezi kuvuna sehemu ambayo hukupanda kitu

Unakumbuka ukiwa shule watu ambao muda wote wanasoma na kushinda maktaba walionekana wanapenda sifa na kuona hawajui kama kuna maisha mengine kama vijana? Kitu gani kilitokea wakati wa mitihani? wasiosoma wanaanza kuwasumbua hao hao waliokuwa wanawaona washamba. Kama unataka kuvuna kwenye jambo lolote lazima uanze kupanda mbegu, kwa lugha rahisi unaanza kuwekeza ili uweze kuvuna kitu.

Some la kujifunza : Sikuzote kumbuka kufanyia kazi matatizo madogo madogo, kwasababu huwezi kujua tatizo lipi ukilitatua litakupeleka bali zaidi. Huwezi kujua utakuwa wapi siku za usoni ila unapoendelea kufanya kitu fulani kaiak maeneo mbalimbali kitu kinaweza kutokea na ukakwea kwenda juu.

3. Badili matatizo yako yanayokuzunguka. Shughulikia vibovu viwe amali yako

Kama unanuia kufanya kitu kikubwa vile vitu ambavyo watu wanadharau unaweza kufanya vikawa amali ya kukusaidia. Watu wengi tunapenda maisha mtelemko au rahisi, hebu fuatilia watu wote waliofanikiwa hawakuibuka tu kutoka sehemu fulani bali waliweza kutatua matatizo yaliyowazunguka na kutoka pale walipo. Unachotakiwa kujua kwamba kwanini unashindwa kutatua jambo fulani na wengine wanawezaje? Watu wengi tunatatizo la kuona hatuwezi na wala hatujui kama tunaweza kutafutia ufumbuzi wa kitu fulani kwahiyo tumebaki na akili mgando ambayo inasubiri watu wengine watutatulie matatizo tulionayo.

Unatakiwa kujua matatizo, kuyatafutia ufumbuzi na  kushughulikia kuyatatua, na hii itawezekana kama una akili ya kitafiti na kushughulikia mambo.

4. Ufahamu na utendaji ni vitu ambavyo vinakwenda pamoja

Huwezi kuwa mtendaji mzuri kama ufahamu wako uko chini au hujui mambo, itakupa shida sana. Watu wengi huwa wanatamani wake watendaji wazuri lakini ufahamu wao wa mambo ni mdogo sana kiasi kwamba hata wakijitahidi vipi matokeo yanakuwa ni madogo hivyo hivyo. Unahitaji kufahamu kwa karibu na kwa undani wake kile ambacho unapaswa kukifanyia kazi. Kwa kifupi unatakiwa kuwa mtu lee elimika kwenye jambo ambalo unataka kulifanya, hii inamaanisha inseam makala mbalimbali kuhusu jambo hilo, utafiti uliowahikufanyika na baada ya hapo utaweza kutendea kazi vizuri hicho kitu. Kuwa mtendaji mzuri unahitaji haiba ya kujifunza sana mambo mengi ili uweze kuyatumia kwenye maisha yako na kazi yako kwa ufanisi mkubwa na kwa mpangilio mzuri wa kueleweka. ukiwa hauna mpangilio wa namna unavyojifunza na utekelezaji wake utakusumbua.

5. Tafuta watu muhimu na matatizo, harafu uwekeze huko. 

Unapotafuta watu muhimu au watu wenye matatizo fulani na ukaweza kuyatatua utajikuta unafikia malengo yako vizuri. Ila usiende sehemu ukauliza hivi ninyi man matatizo gani? wengine wanaweza wasikukalibishe tena, njia rahisi ya kujua matatizo ya watu au kitu fulani jingo ukaribu nao na shirikiana nao kwa ukaribu utajua matatizo yao ndipo utaweza kujenga mbinu mbadala wa kutatua shida hiyo. Hiyo we kwenye taaluma yako yoyote ukiweza kuwa mbunifu namna uanavyojishughulisha katika kushungulikia shinda na matatizo watu wengi watakuamini na kufanya kazi na wewe vizuri.  Hivyo unatakiwa kujiuliza je ni tatizo gani unalotaka kulishughulikia? Unapotafuta uvumbuzi wa tatizo usiruhusu kitu chochote kikuharibie mpango na mikakati yao, ongeza umakini mkubwa katika utendaji wako. Mafanikio hayataacha kukufuata.

6. Fanya kazi na watu wengine kwa moyo mweupe.
Unapofanya kazi na watu wengine usiruhusu kiburi na kujiona bora kuliko watu wengine vikatawala eneo lako la kazi au watu wanaokuzunguka. Mara nyingi watu tunakosea tunajaribu kuwadidimiza watu wanaotuzunguka ili tuweze kwenda juu au kufanikiwa hivyo tunaishia watu kutukimbiana sisi wenye kupata msongo wa mawazo mambo yasipoenda vizuri. Kama unahitaji kufanikiwa amali kubwa uliyonayo ni namna gani unaishi na watu wanaokuzunguka? je umewekeza kiasi gani kwa hao watu na je wanauwezo wa kukusaidia hapo mbeleni? Watakuwa msaada kwako kulingana na vile ambavyo unawatenda kila siku.