Je CV yako imebeba kitu gani?

0
182 views

Mwajiriwa mpya au mtarajiwa CV yako ni kama duke lililowazi hivyo mnunuzi anaweza kujua kama kuna kitu ndani kinachomfaa au hakuna. CV yako inatakiwa we imepangiliwa kwa mtindo ambao unamvutia mtazamaji au msomaji, hivyo we rahisi na inayoeleweka kirahisi.

  1. Habari zako binafsi na mawasiliano yako. Hapa utajumuisha yafuatayo:
    (1) Jina Lako Kamili (Jina lake la Kwanza, ikifuatiwa na Jina la katikati ,na mwisho jina la ukoo au Familia), (2) Anuani ya Posta ilea kamili (Unaweza kuweka anwani ya chuo unachosoma kama bado inseam au anwani ya nyumbani), (3) Mawasiliano yako ya simu na muda ambao mawasiliano yako huwa yanapatikana , (4) barua pepe (ili waweze kuwasiliana na wewe kwa njia ya mtandao).
  2. Maelezo ya Elimu na Ufaulu. Hapa unahitaji kuonyesha shule na vie ulivyosoma, masomo uliyosoma na namna ulivyofaulu na kiwango cha ufaulu
  3. Uzoefu (Hii inahusisha kazi ulizofanya kwa muda mfupi au kuajiriwa kabisa) Inahusisha Jina la Kampuni, Anwani yake, kazi uliyofanya na kwa ufupi majukumu ya kazi hiyo au hizo.
  4. Mafanikio Hapa zingatia mafanikio ambayo yanaeleza ushahidi wa uwezo kama ulivyoainisha.
  5. Interests (Kitu kinachokutofautisha wewe binafsi) hapa zungumzia utofauti wako katika utendaji na namna ambavyo unaweza kujifunza vitu katika mazingira tofauti.
  6. CVs Zinatengenezwa kwa mfumo fulani ili kuweka habari zinachohitajika kwa haraka na kwa urahisi kwa ajili ya msomaji.
    Hili jambo ni muhimu kwa sababu kuna mama ya watu kila siku wanatuma CV zao kwa ajili ya kutafuta kazi. Hivyo basi msomaji anajua wapi atapata habari annoy ihitaji hivyo ukiandika na kuweka sehemu tofauti anaweza asiendelee na Cv yako. Kwa ujumla ni kwamba Cv inafungua habari zako binafsi na mawasiliano yako, ikifuatia na historia ya elimu yako pamoja na afoul wako, Mafanikio yako na mwisho ni interest(kitu kinachokutofauti wewe binafsi) yako.Unaweza kujitofautisha na mfumo huo wa namna ya kuandika CV lakini kuna gharama inaweza ikakupata. Moja ya Gharama hizo ni kutosomwa kwa CV yako.