Makosa wanayofanya viongozi wabaya yanayofukuza wafanyakazi wazuri

0
209 views

Kama unataka watu makini na wazuri kwenye kampuni yako waendelee kufanya kazi na wewe, inakubidi uwe makini kwa namna ambavyo unawajali na kuwatumia.
Vitu ambavyo ni gharama sana hasa kwenye kampuni yako ni pale wafanyakazi bora wanapoamua kuondoka kwako.

Kuna watendaji hasa ngazi ya mameneja wanalalamika kwa habari ya wafanyakazi bora kuondoka, na wao wanaishia kulalamika. Wengi huishia kulalamika kwanini wanaondoka, kitu ambacho unapaswa kujua ni kwamba watu wengi huwa hawaachi kazi kwa sababu ya kazi yenyewe ila kwasabu ya wanawakimbia mabosi zao.

Cha kuhuzunisha ni kwamba jambo hili linaepukika kwa njia rahisi sana. Kinachohitajika ni kupata mtizamo mpya unapowaongoza watu wengine.  Kampuni linajua umuhimu wa wafanyakazi wanaohamasika katika kazi zao, lakini wanashindwa kuwawajibisha mameneja kuhakikisha watu wamehamasika kazini.

Kuna utafiti umefanyika kwamba wafanyakazi waliohamasika walikuwa asilimia 33 ya uzalishaji zaidi, na mauzo asilimia 37 zaidi ya wale ambao hawajahamasika. Vile vile wafanyakazi hao hao waliohamasika asilimia 87 walikuwa hawana mpango wa kuacha kazi au kutafuta sehemu nyingine. Idadi ya watu waliofanyiwa utafiti huo ilikuwa ni elfu hamsini (50,000).

Utafiti mwingine unaongeza na kusema kuwa wafanyakazi waliohamasika na wanaofanya vizuri kazini ni kwa sababu ya bosi aliye juu yake, Hebu sasa tutazame vitu ambavyo mabosi wengi wanafanya kuwafukuza wafanyakazi.

1. Kuwafanyika kazi nyingi na masaa zaidi.
Hakuna kitu ambacho kinawachosha kama kuwatumia vibaya. Mara nyingi watu huangukia kufanya kazi kwa juhudi na maarifa mengi ili wapate matokeo mazuri lakini kuwatumia wafanyakazi vibaya ukipisha muda wa zaidi masaa 50 kwa wiki utendaji huwa unapungua hivyo ufanisi unashuka zaidi.

Kama unataka kuongeza kazi kwa wafanyakazi wako na wenye vipaji, waongezee na nyadhifa vile vile. Wafanyakazi bora wanaweza kufanya kazi zaidi lakini hawawezi kuvumilia kama kazi hiyo inawaumiza kila kukicha. Namna nyingine ya kuwaongezea kazi ni kuwapandisha vyeo, na mishahara yao kuongezeka. kama unawapa majukumu na kuongeza majukumu bila kubadirisha hali zao watatafuta kazi nyingine ambao wanaona watathaminiwa zaidi kuliko unachowafanyia.

2. Kutothamini mchango wao na kazi nzuri wanazofanya.
Ni rahisi sana kudharau au kusahau kumpongeza mtu anapofanya vizuri na ukaendelea kumpa kazi nyingi zaidi. Bosi mzuri anatakiwa kuwasiliana na wafanyakazi wengine na kujua wanafurahia kitu gani, wengine wanapenda shukrani ya pesa, wengine kusifiwa mbele za watu n.k kama mkuu wao wa kazi lazima utafute namna ya kuwapongeza ambako kutawafanya waendelee kufurahia kuwa chini yako na huku kazi na malengo yanafikiwa.

3. Kushindwa kuwaendeleza kitaaluma.
Mabosi wengi wakiulizwa kwa nini hawawasikilizi wafanyakazi wao, wanajaribu kukwepa kwa kusingizia vitu kama “kukosa imani nao” “hataki kuzoeleka hovyo” hivyo vote haviongezi chochote. Bosi mzuri anatawala vizuri, na ni msikilizaji mzuri kwa watu waliochini yake.

Utawala unaweza kuwa na mwanzo lakini inaweza kuwa haifa mwisho. Unapokuwa na wafanyakazi, bora , wabunifu na wenye vipaji, ni kazi yako wewe kutafuta maeneo ambayo unaweza kuwaongezea taaluma na ubunifu kukua zaidi. Wengi wa wafanyakazi wanataka mrejesho wako zaidi ya wale ambao bora liende. Ni kazi yako wewe kama mkuu wao wa kazi kuhakikisha kwamba unawasiliana nao na wanajua kila kinachoendelea.

4. Kutowajali wafanyakazi wao.  Nusu ya watu ambao huacha kazi kwenye mashirika na makampuni mengi ni uhusiano walionao na wake wao wa kazi. Makampuni makini yanaweza uwiano kati ya kazi na maisha ya mtu binafsi. Kuna mabosi ambao hufurahia mfanyakaza ambaye anafanya vizuri, kuwafariji wale ambao wanapitia mambo magumu au changamoto na kuwapata changamoto hata kama inauma. mabosi ambao hawajali mtu na maisha yake hukimbiwa sana, kwasababu ni ngumu kufanya kazi na mtu ambaye unaishi naye masaa 8 kila siku, halafu hamjaliani kwa jambo lolote zaidi ya kukutaka ufanye kazi kwa moyo wote.

5. Hawatekelezi ahadi zao wenyewe. Kuwapatia watu ahadi kunakufanya unawake watu katika hali tete kati ya kukufurahia au kuondoka. Unapoweka ahadi kwa wafanyakazi uvaongeza tumaini la hao watu kwako na pindi utakapo tekeleza ahadi yako uonaongeza uamnifu. Wafanyakazi wengi huwaamini mabosi ambao ni watekelezaji wa maneno wanayotamka na kuyaahidi. Kushindwa kutekeleza maneno uliyoahidi, unajipotezea au kujipunguzia heshima na watu wanaachfa kukuamini.

6. Huajiri na kupandisha vyeo watu ambao si sahihi. Watu wazuri, wanaofanya kazi kwa kujituma wanataka kufanya kazi na watu wenye taaluma inayofanana na ya kwao. Wakati mabosi hawatumii nguvu na juhudi kuajiri watu ambao wanaijua tithing walioingia wanawakatisha tamaa wale wengine ambao ni watendaji wazuri. Vile vile kuwapandisha vyeo watu ambao si sahihi ambao kila mtu anajua kwamba hawana huo uwezo wa kupandishwa vyeo halafu wakapandishwa vyeo. Huko ni sawa na kuwatukana wanaostahili na ni sababu ya wengine kuondoka. kama huna mpango wa kuwapandisha vyeo wanao stahili basi hata hao wasiostahili waache hivyo hivyo.

7. Hawapendi kuona watu wanafanya wanachokipenda. Wafanyakazi wabunifu wanapenda kufanya vitu fulani. Kuwapa furs ya kufanya hicho ndio kitu muhimu na pekee ili waendelee kukaa kwako. Wanapofanya wanachokipenda  kunawafanya wajisikie kuridhika na kuongeza utendaji kazi wao. Mabosi wengi wanafikiri utendaji wao utashuka kama wakifanya vitu wanavyovipenda, ingawa hofu hiyo haina ukweli ndani yake, kwa sababu utafiti unaonyesha kwamba wafanyazi wabinifu wanapofanya wanachokipenda inawaongezea uwezo wao mara tano (5) zaidi.

8. Wanashindwa kujiingiza kaka ubunifu. Wafanyakazi bora na wabunifu wanataka kuboresha kila kitu kinachopita mikoni mwao. Kama ukiondoa uwezo wao wa kuboresha na kubadirisha mambo inamaanisha wewe unapenda cheo tu na kuwafanya kuchukia kazi yao. Kuwafungia na kuwazuia kunakupunguzia wewe kukua na si wao maana wao wanatafuta sehemu nyingine ya kwenda coynessha uwezo wao.

9. Hawawapi changamoto wafanyakazi wao kisomi. Mabosi wanaojielewa huwapa changamoto wafanyakazi wao kwa kuangalia uwezo wao kitaaluma. Badala ya kuongeza majukumu na kufikia viwango vipya vya utekelezaji wao huwapa nguvu na kuwasaidia kufanikisha kazi hiyo. Wafanyakazi wengi ambao wana uwezo mkubwa wakikuta wanafanya kazi zile zile na wala hakuana changamoto katika taaluma yao, wanatafuta kazi nyingine ambayo watafurahia kuifanya kutokana na changamoto zake.

Kama unataka watu wako waendelee kukaa katika kazi ambazo umewaajiri, fikiri kwa makini namna ambavyo unawatawala. Wafanyakazi wazuri wanaochapa kazi na wenye vapid wana nguvu ya kutokata tamaa, ujuzi wao unaware ubunifu mwingi wa wutatua changamoto wanazokutana nazo. Unahitaji kuwafanya waendelee kufanya kazi na wewe.