Unatakiwa Kuvaaje unapokwenda kwenye Usaili?

0
152 views

Uvaaji wa wafanyakazi wazoefu na wapya wanafanana katika mwonekano na namna ya uvaaji wao. Mashirika mengi yanaweka umuhimu katika mavazi ya kiofisi ambayo yanaashiria mwonekano bora kwa wafanyakazi wake. hakuna shirika au kampuni ambayo inapenda kuona watu wake wanavaa mavazi ya ajabu na yasiyokuwa na mwonekano wa heshima kwa jamii na wateja wake.

 1. Umuhimu wa mavazi na mwonekano vile vile unategemea aina ya kazi ambayo unafanyiwa usaili.
  Unapokwenda kwenye usaili unaohusisha kazi ambayo ni ya kwenda kuonana na wateja au wateja watarajiwa, basi mavazi lazima yawe yenye heshima kubwa, utanashati wa hali ya juu. Wanaokufanyia usaili wanapokuangalia huo unakuwa mwanzo wa kukuangalia ingawa kama watakuchukua wana matarajio makubwa katika utendaji wako wa kazi kulingana na kazi uliyoomba na wanaangalia hata ukipanda cheo utakuaje. hivyo hutizama malengo ya muda mrefu pia.
  B9693_WB6622_m
 2. Vaa mavazi ambayo utaendelea kuvaa kama watakuajiri. Inamaanisha usivae kitu ambacho hutakuja kuvaa tena mara baada ya kupata kazi.
 3. Usipake wanja na mikorogo mingine kupita kiasi. Unatakiwa uonekane wewe kama wewe, umaridadi wako wa kikazi zaidi na sio kama unakwenda kwenye kumbi za starehe. Kwa wadada hutakiwi kuvaa viatu virefu sana au flat, inatakiwa viwe vya ulefu wa kati ambao unakuongezea ujasiri unapotembea na kuongea na mtu. Nguo za kuonyesha mabega, kifua kuonyesha mwanzo wa matiti hivyo vyote haviruhusiwi kwani vinakuwa vinawaletea picha tofauti wale ambao wanakufanyia usaili.
 4. Je mwonekano wako wa kwanza kwa watu wengi unaleta picha gani kwao?
  Mwonekano wako wa kwanza ni muhimu sana kwa mtu ambaye anategemea kukuajiri, ukipoteza fursa hiyo ni mara chache sana kwamba utapata nafasi ya pili ya kusahihisha makosa yako.
 5. Ogopa kuvaa kawaida sana au kujirahisisha.

Sababu yake ni kwamba mtu anayekufanyia usaili anaangalia ukifika kazini utakuwa mtu wa namna gani. Ukionekana kirahisi rahisi na hauna mpangilio mzuri kwenye mavazi, wanaweza wasikupe kazi kwani inaonekana hutakuwa na mwonekano mzuri kwa wateja wao.

6. Kama hujui namna ya kupangilia mavazi fanya utafiti.
Hebu jaribu kujua kwamba wewe ni mtu wa aina gani na unataka kwenda wapi na uwe na mwonekano gani. Kama unataka kuwa kwenye nyazifa za juu, kuna mavazi yake na na uvaaji. Kitu cha msingi unatakiwa kutafiti shirika hilo unaloliendea kufanya usaili wanapendelea nini na mwonekano wao ukoje. Hutakiwi kukurupuka katika eneo hilo.