Ujuzi wa kuwasiliana ambao utakusaidia kuishi na watu wengine vyema

0
289 views

Uongozi kwa namna nyingine ni mawasiliano kati yako na walio chini yako vile vile kati yako na walio juu yako, unahitaji kuwa na ujuzi mahususi katika nafasi yako ya uongozi.

Unapokuwa unaongoza watu iwe ni ofisini au nje ya ofisi, kwenye taasisi za kuajiliwa au taasisi ambazo watu wanajitolea kufanya kazi, Mawasiliano mazuri yanakutofautisha na watu wengine. Kuna watu wengine wameumiza watu waliochini yao au kuwafanya watu wengine wasiweze kufanya kazi zao sawasawa kwa namna mbaya ambavyo wanawasiliana na hao watu.  Unatakiwa kujua kwamba mawasiliano yanaongeza molali ya mtu kufanya kazi au hupunguza molali hiyo inategemeana umewasiliana naye kwa namna gani.

1. Unatakiwa kujitambua

Mawasiliano mazuri yanatokana na wewe mwenyewe kujitambua vizuri hasa unapowasiliana na watu wengine. Jifanyie utafiti binafsi kujua je mawasilano yako yanaathiri vipi utendaji wa watu walio chini yako? watu wanakusoma vipi katika kauli zako, jaribu kuwa makini kwamba watu waste winsome sura yako kwamba leo uko kwenye sura fulani au ya kumuadhibu mtu, au kukasikika bila sababu katika kauli zako ili usijikute unapeleka hasira zako kwa mtu mwingine ambaye ahusiki na kile unachokizungumza.  Mawasiliano mazuri unapojitambua unajua neno gani linapaswa kusema kwa nani na kwa wakati gani na sio kuropoka ropoka tu bila mpangilio.

2. Unapaswa kuwatambua wasikilizaji wako.

Kama kiongozi una watu unaowaongoza hivyo basi maneno yako yanaathari kubwa kwa watu unaowaongoza. Kwa namna nyingine ni kwamba unavyowasiliana na mtu alive chini yako unahitaji kujua uwezo wao wa kufikiri na kupokea hicho unachowasiliana nao bila kuathiri ujumbe husika. Wape nafasi ya kuwa huru wanapowasiliana na wewe ili uweze kuwaelewa zaidi.Usitumie lugha ngumu wao kuelewa, kumbuka dhana ya kuwasiliana nao ni kuongeza ufanisi katika utendaji, iwe ni mawasiliano ya kawaida au ripoti za utendaji na namna ya kuwapa majukumu hakikisha wanaelewa unachokitaka na kinachotakiwa kufanyika.

3. Uwe muwazi na ueleweke. 

Viongozi wengi wanapenda kutoeleweka au wanaongea kwa lugha ngumu kueleweka na watu waliochini yao. Kumbuka kwamba watu hufanyia kazi kile walichokilewa, hivyo hutakiwi wewe kama kiongozi kutoa maelekezo ambayo yako pungufu au hayaeleweki na hayajulikani unakusudia nini na wapi kwa mtu gani au idara gani. Ni vizuri urudie kuelekeza zaidi na zaidi na uhakikishe umeeleweka kabla ya kuondoka chumba cha mikutano au kbla mtu unayemwelekeza hajaondoka ofisini kwako. Tumia lugha rahisi na inayelekeza kitu gani kifanyike na kwa hatua zipi hasa na kwa muda gani na wewe mwenyewe ujiridhishe kama ni wewe ungekuwa unafanya ingekuchukua muda gani?

4. Uwe makini na lugha au mawasiliano ya vitendo 

Watafiti wanasema lugha ya vitendo ni muhimu sana kama tu na vile mtu anavyoongea. Mfano sura anavyoinyesha, mikono anavyoichezesha, pamoja na macho yote kwa pamoja yanaonyesha kwamba  mtu unayeongea naye anakubali kile unachomwambia au anadharau ujumbe wako.
Pale unapoongea na mtu uwe makini vile vile na mwili wako mwenyewe kwa namna ambavyo unaonyesha sura yako, mikono yako na hata macho yako ili kile unachokiongea kiendane na lugha ya vitendo kwenye mwili wako mwenyewe unakuwa unamsaidia yule anayekusikiliza kuwa na uhakika na kitu unachokimaanisha.

5. Jifunze kuwa msikilizaji mzuri.

Moja ya nzia bora za kuruhusu uwazi na ukweli kwenye mawasiliano katika kundi la watu ni uwezo wa wewe kujifunza kusikiliza. Mtu anapoongea na wewe sikiliza wanachokwambia kwa makini na wakimaliza kuongea unaweza kuuliza swali kuonyesha kwamba ulikuwa unafuatilia walichokizungumza na kuhakikisha kwamba hujamwelewa vibaya. Uwezo huu unakuongezea uwezo wa wewe kusikilizwa na kuwasikiliza watu wengine.

6. Uwe na mawazo chanya na mwenye heshima. 

Hii haitakiwi kwenda kwamba kwa bahati mbaya hii huwa haiwi hizi au sidhani kama itawezekana. Zingatia uwazi, ukweli na kuheshimu mawazo ya watu wengine kwani itakuongezea motisha wewe na wale ambao unawaongoza. Usikimbilie kusema kuwa jambo haliwezekani au kila wakati wanapotoa mawazo yao unakuwa na mlengo hasi na wewe ndiye unayejua kila kitu, hiyo inaathiri wale unaowaongoza.

Kila mawasiliano yanaelezea kitu kinachoendelea, hutaweza yote haha kwa siku moja bali unatakiwa kujifunza na kuweka katika majaribio kila wakati kwa kudhamilia mwishowe utajikuta mawasiliano yako yamekuwa bora na watu wanafurahia kufanya kazi na wewe. Utakapofikia kiwango hicho utashangaa kwamba watu wanaofanya kazi chini yako wanaufanisi mkubwa sana ukilinganisha na pale ambapo ulikuwa hujui namna ya kuwasiliana kwa njia bora zaidi.