Kitu gani watu wasiochoelewa dhana ya kupata kipato huku ukiwa nyumbani

0
162 views

Dhana ya kujiptia kipato ukiwa umekaa nyumbani imepotoshwa kwa kiasi kikubwa hivyo kusababisha using hata kati ya wasomi wetu ambao tunategemea kuliendesha taiga hili. Watu wameshindwa kutofautisha utapeli wa kwenye mtandao na kufanya kazi ukiwa nyumbani.Kufanya kazi ukiwa nyumbani hicho kitu kinawezekana, hasa kwa kazi ambazo hazikuhitaji moja kwa moja kuwepo ofisini ili kazi ifanyike, mfano. Mwandishi wa habari wa kujitegemea, hahitaji kuja ofisini kuripoti kila siku saa mbili asubuhi. Yeye atakachofanya ni kukutumia habari yake kwa njia ya barua pepe au kwenye mfumo wenu wa kupokelea habari kisha inakwenda kwa mhariri na baada ya hapo watu wataisoma kwenye vyombo vya habari kama magazeti n.k.
 chayanne-885227Kazi nyingine kama kufanyia kazi takwimu zilizokusanywa, kusimamia tovuti, kuwekeza kwenye masoko ya hisa yanayoeleweka, wabunifu wa mitindo, watengeneza program za kompyuta, wapokea simu za huduma kwa wateja, wabunifu na waandaaji wa matangazo ya picha na hata video. wanaweza wakafanya kazi mahali popote na kufikisha kazi zao kwa nia ya mtandao kwa mhusika na kujiingizia kipato. Inamaanisha mtu huyo yupo nyumbani rakini anafanya kazi inayomhusu bila kuathiri utendaji wake. Kuna watu wanadhani wanaweza kukaa nyumbani na hela ikaingia tu, kwa kujiunga kwenye mfumo fulani hivi.

Habari mbaya ni kwamba, wacheza upatu wamepotosha dhana ya kufanyia kazi nyumbani

Wacheza upatu wakubwa duniani wamekuja na njia ambazo wanakuhakikishia kwamba utapata hela kila wiki, kwa kuwekeza kwenye mifumo yao waliyoitengeneza kwa lugha ya uwekezaji hivyo kupata fedha chap chap. Jamaa hao wanachofanya ni kuwarubuni watu wachache na kuwalipa ili waonekane kwamba hicho kitu ni halisi lakini mwisho wake watu hupoteza mali zao.

Hao ni matapeli kama matapeli wengine, tamaa yako ya utajili wa chap chap ndio utakaokupoteza na kukupelekea kuingia matatizoni. Hakuna mfumo ambao unaweza chukka marejesho ya uwekezaji kwa kiasi kikubwa kama hicho unachoambiwa. Matajiri wengi ukiwauliza walipataje utajiri wao , utashanga kwamba hawajapitia using huo ambao watu wanarubuniwa nao na wengine ni wasomi kabisa ila akili na ufahamu wao umefugwa.

Habari nzuri ni kwamba hakuna mtu ambaye anakupenda kiasi hicho cha kukupa fursa wewe uingize hela kwa kiasi hicho, ndio maana matajiri wa hapa kwetu hawajawahi kukutangazia kwamba kuwekeza kwenye ramba ramba kunalipa, au mikate, au unga wa sembe na chapati kila siku wanaboresha na kuja na mbinu mpya ili biashara zao ziendelee. Wanajua kabisa hakuna hela rahisi rahisi kama unavyodhani, kitu cha msingi unachotakiwa kufanya ni kuwa mbunifu an kufanya kazia halisi za kukuingizia kipato achana na njia za mkato.