TABIA ZINAZOFANYA BIASHARA YAKO ISIENDELEE

0
166 views

Kuna tabia mbaya ambazo ni za kawaida au tumechukulia ni kawaida na kutolea sababu kwanini tukonazo hizo tabia.

Wengine huwa wanasema kwamba wao wanafikiri sana kabla ya kufanya maamuzi lakini ukweli ni kwamba wanakwepa mabadiriko. Kuna wakati mwingine utasema mimi ni wamuhimu sana ninachagua barua pepe za kujibu na kwamba una mambo mengi lakini ukweli ni kwamba ni mvivu kwani kusoma hiyo barua pepe itakuchukua muda gani?
Usijidanganye, sababu hizo zitakuletea madhala makubwa kwenye biashara yako. Ukiendelea na tabia hizo, ndoto ya mafanikio itakuacha mbali sana,

  1. Unahitaji mabadiriko kwa Namna unavyopokea Ushauri
    Kama umekuwa ukiendesha biashara yenye mafanikio kwa muda Fulani unajikuta kwamba unafika mahali unapinga mabadiriko.

Unajiuliza kwanini nifanye kitu kingine wakati biashara inaendelea vizuri? Hayo ni mawazo hatari sana kuendelea kufanyia kazi, kwasababu ili biashara iendelee inahitaji kujifunza na kubadirika kila wakati katika maamuzi.
Kama wafanyakazi wako wakija kukupa ushauri na hali halisi ya biashara inavyokwenda, je unawapotezea au unafanyia kazi wanachokisema? Au wakishasema unaanza kuwaambia namna gani ni gharama kufanyia kazi hicho wanachokisema hata kabla ya kujua kwamba kina faida kiasi gani? Ukiendeleea kupuuza mawazo yao muda si mrefu au walishaacha kutoa mawazo yao kabisa na wanafanya kama kawaida. Wakati wote wewe kama mjasiriamali na mfanya biashara unatakiwa kuwa na ufahamu wa kujaribu mbinu tofauti tofauti na matokeo yake yaweze kukusaidia kufanyia maamuzi

2.Watu wengine kwa juhudi wana wasiliana na wewe lakini hawapati majibu au Ushirikiano wa Kutosha  kutoka kwako.

Inapotokea hali kama hiyo jaribu watu hujiuliza ni kwamba je una mambo mengi sana kiasi kwamba huwezi kujibu au wao si wa muhimu kwako?

Uhalisia ni kwamba siku hizi watu wengi wanaenda na simu zao hata bafuni ili wasikose chochote. Hivyo basi ujumbe wao wa maneno lazima unauona lakini unaamua kupuuzia. Hii tabia inawafanya watu kuanza kukaa mbali na wewe, kwani ni gharama kiasi gani kujibu? Usiwafanya wajiulize maswali mengi kwamba haujali.
Ni kweli kwamba kuna fulsa nyingine zimepitwa na wakati, lakini fikiri kwa haraka na kujibu haraka kila ujumbe unaopata wa kibiashara itakusaidia kupata habari nyingi zaidi kwani watu watajua wewe si mpuuziaji na hiyo itasaidia biashara yako.

  1. Haujali mambo yanayoendelea

Wajasiliamali wengi wanakuwa wanasingizia mambo mengi hivyo wanajikuta hawaendi na wakati uliopo na kushindwa kujua mambo yanayoendelea. Kama mjasiliamali unatakiwa kujua mambo yanayoendelea kibiashara kwa kusoma kwenye magazeti, mitandao ya kijamii na hata tovuti mbalimbali ili kupanua wigo wako wa kibiashara na kujua fulsa zako zinaendana na mazingira kwa kiasi gani. Usipuuzie kutafuta muda wa kukutana na watu kwenye jamii na wafanya biashara wenzako kwenye mikusanyiko inayohusu biashara.

Unajikuta unapuuzia teknologia inavyobadirika hivyo hutaki kubadirika, biashara inawezakufa kutokana na aina ya mtizamo ulionao. Je mtizamo ulionao unamanufaa kwa biashara yako au ni nyenzo ambayo itaua biashara hapo baadaye?

4. Unajiendeleza kiasi gani kwenye elimu ya biashara?

Watu wengi hawapendi kusoma hivyo kile walichokipata miaka kadhaa iliyopita wanaona kinatosha kuwapeleka mpaka mwisho. Mtizamo huu sio sahihi, biashara inabadirika na vitu vingi vinabadirika lazima ujiongezee ufahamu kila iitwapo leo ili usipitwe na wakati kwenye biashara yako. Unatakiwa kujiuliza nje ni elimu gani inahitajika ili niboreshe kile ninachokifanya kila siku? na elimu hiyo ninaipataje?

Hivyo basi kwa ufupi ni kwamba maendeleo ya biashara yako yanategemea sana tabia na mtizamo ulionao kwenye biashara na watu wanokuzunguka. Hakuna mtu anajua kila kitu, unahitaji watuu wengine kwa namna moja ama nyingine katika maisha yako na maisha ya kibiashara.