Je unafanyeje wateja waendelee kurudi kwako?

0
225 views

1. Bei yako inatakiwa kuwa juu kidogo ya jirani yako

Bei huonyesha thamani ya huduma unayofanya na wengine bei ikiwa kubwa inaonyesha thamani ya bidhaa hiyo iko juu. Unapoweka be ya bidhaa au huduma chini ukifikiri kwamba ni kitu ambacho wateja wako watakiweza wakati huo huo wengine watadhani ubora wake umeshuka. Matokeo yake itakuwa baadhi ya wateja watakwenda sehemu nyingine ambayo wanadhani ubora na uthamani uko juu zaidi yako.

2. Onyesha umahili wako katika biashara.
Ujasiri na umakini ni moja ya vitu vinavyoongeza kufanikiwa kwa biashara. wateja wanakuja kwako wakiamini wewe una weredi wa hicho unachokiuza. Ukionyesha kuwa na macaque au wasiwasi au kusitasita haraka watatafuta mtu anayejua kuhusu kitu anachokiuza.
Hivyo basic hata kama huna ujasiri ndani yako inakubidi uongeze ujasiri huo ili kuwashawishi wateja wako.

3. Ongeza thamani ya huduma
Usipende kutoa huduma za viwango vile vile ambavyo ulianza navyo. Wateja wanataka kuona kuna ongezeko katika ubora na katika huduma. Unahitaji kuwa mbunifu wa hali ya juu kufikiri zaidi ya mteja na unamfanyaje aweze kurudi tena na tena na tena. Kumbuka kuwa mteja akiridhika na kufurahia huduma yao au bidhaa yako ni rahisi kupata mteja mwingine kutokana na wateja wako hao hao.

4. Kionjo cha siri= kutoa ofa mara kwa mara
Kumbuka unapouza au kutoa huduma halafu mara nyingine ukatoa ofa. Wateja watakupenda bure, kama unakumbukumbu zuri miaka michache iliyopita ukitaka kusafiri kwenda mikoani kulikuwa na mabasi ambayo ukiingia utapata soda, maji, peremende na biskuti na walipata wateja kuliko wenzangu na mimi waliokuwa hawawezi kuongeza kionjo katika usafiri. Unapoweza kutoa ofa hata kama si kubwa sana watu watawaambia rafiki zao na watawambia watu wengine.

5. Siku zote waelimishe wateja wako
Unapofanya biashara na wewe ndive unayeijua bidhaa hivyo unahitajika kuwaeleimisha mteja kwa usahihi. Kitu ambacho unatakiwa kuwa wa tofauti katika huduma na bidhaa zako. hata siku moja usije ukajaribu kumdanganya mteja wako, mteja ataridhika na kurudi kwako kila wakati.  Kitu gani kinakufanya wa tofauti? je huduma yako inatofauti ipi? kwanini mteja arudi kwako wakati mwingine? Ukiweza kumjibu mteja maswali hayo utamfanya kurudi kwako kila wakati.

6. Kusanya Ushahidi wa kijamii.
Unaweza ukajiuliza ushahidi gani au ushahidi wa nini? umeshauza bidhaa mwache akahangaike nayo, hapana tafuta wateja ambao wamenuafaika na bidhaa yako au huduma yako na huo ndio ushahidi na kuonyesha ubora wa kitu unachokifanya. Weka ushahidi huo kwenye picha za video na sauti na hata picha za kawaida halafu waonyeshe wateja wako na wateja watarajiwa kwenye mitandao ya kijamii kupitia ukurasa wako wa biashara hiyo.

7. Usiombe Msamaha bila kumshungulikia mteja tatizo lake.
Kuna vitu vingi hutokea unapohudumia wateja, usiwe mwepesi wa kuomba msamaha kwa kitu kinapotokea ambacho kinahitaji weredi wako, kinachotakiwa uwe jasiri na wala usipoteze mwelekeo jambo linapotokea tafuta njia ya kulitatua ili mteja aridhike ndipo uendelee na mambo mengine. Hapa simaanishi umefanya kosa la hasa, ni makosa ya kupaki bidhaa au mteja alionekana kushangaa namna alivyopewa bidhaa n.k Onyesha unajali na kumhudumia kwa namna ya tofauti na mategemeo yake, ikitokea unahitaji kumwomba msamaha fanya baada ya kumaliza kushughulikia tatizo lake wakati wa kumkabidhi hiyo huduma au bidhaa.

Kumbuka mteja ni mfalme, yeye ndiye anayesababisha maisha yako yaende mbele mhudumie kwa umakini mkubwa.