Je unajua kitu kinachoitwa mwelekeo?

0
92 views

Je unajua kitu kinachoitwa mwelekeo? Mwelekeo ni kujua wapi unapaswa kwenda au kuona njia inayokuongoza, hivyo haimaanishi lazima ujue unakwekwenda. Unaweze kuwa unakwenda kwa sababu ndo njia pekee au ndo mwelekeo pekee unaoujua.

Vivyo hivyo katika taaluma unahitaji maono (vision) ya kujua unakoelekea ili usipoteze muda na kufanya kitu tofauti ni zaidi ya kuwa na Stashahada au Shahada ya kitu Fulani. Inawawezekana neno maono likakuchanganya kwa sababu huwahulisikii mara nyingi kwenye masikio yako. Maono ni uwezo wa kujua mambo yaliyombele vile unavyotakiwa uwe. Hivyo Basi ukiweza kuona mbali kila mpango utakaokuwa ukifanya utauelekeza kule ulikoona unatakiwa ufike.

Suala ni kwamba unataka kuwa nani miaka kumi au ishirini ijao kama utakuwa Hai? Watu wengi husema itategemeana na hali inavyokwenda, na hicho ndicho kimeendelea kugharimu kwenye mfumo wetu wa maisha hata nchi kwa ujumla. Vitu vingi tumeshindwa kuviwekea maono na sasa tunashangaa kwanini mambo yako kama yalivyo. Tunachojaribu ni kushughulikia na kufanya zima moto katika mambo ambayo yalitakiwa yawe yameshughulikiwa muda mrefu sana.

JE UNAJUA KITU KINAITWA MWELEKEO.